hassan

MISINGI YA TAIFA HUANZIA KATIKA FAMILIA
[Malezi ni jukumu la kila mmoja wetu]

Ni kweli kwamba katika jamii yeyote mtoto ni kitu cha kujivunia sana kwa wazazi walioamua kuwa na watoto.Na ndio maana familiaa ikikosa mtoto inakosa furaha na amani na wakati mwingine ndoa kuvunjika.

L akini kwa upande wa pili inakua kinyume kwani wanaopata watoto bila kutarajia mwisho wake ni kuwatupa chooni
au kwenye dampo ya takataka. Katika kudhiditi utoaji wa mimba zisizotarajiwa hususani kwa wasichana wadogo.mbinu mbalimbali zinazotumika kama anavyoelezea mtaalamu wa masuala ya Afya Dar-es-salaam.

”Kwetu sisi Madaktari, hilo linatushinda kwasababu hivi wanajipima wenyewe kwa kutumia vidonge PrimolutiN vinavyotoa mimba kuanzia ya wiki moja hadi mwezi mmoja, ”alisema mtaalam huyu.
Mtoto yeyote wa kike au kiume ana haki ya kupata lishe bora tangu akiwa mdogo,maziwa ya mama,uji,juisi ili aweze kuwa na afya bora.
Si kula vizuri tu,ila na malezi bora yanamsaidia mtoto kukua katika maisha ya uadilifu ambapo anatakiwa ajue wajibu wake
yeye kama mtoto.Hii ikiwa ni pamoja na kujua yeye ni mtoto na anatakiwa kuwaheshimu wakubwa ambao pia nao wanatakiwa kuwaheshimu watoto na kuwasikiliza.

Pamoja na malezi bora anayopewa mtoto muda wa kucheza na wenzake ili aweze kuwa na furaha,ambayo inamsaidia kukua kiakili tofauti na kumfungia ndani mwenyewe kwa mtoto anachelewa hata kuongea.

Kutompa mtoto malezi bora kunamsababisha mtoto kutokuwa katika hali ya uadilifu na kuwa mjeuri asiye na heshima kwa wakubwa hata watoto wenzake.pamoja na wale wanaolelewa na wafanyakazi wa wandani tangu utoto kutokana na wazazi wao kuajiriwa.

Wazazi wasioopatana wenyewe kwa wenyewe ugomvi kila siku pia wanawalea watoto katika hali inayowaathiri sana watoto wanakuwa wakiwaona wanavyopigana na kugombana hii inawaathili watoto katika kukua na hata baadaye wanaona ni maisha ya kawaida na kunauwezekano mkumbwa wa kuyaishi wakiwa na familia zao baadaye.

Katika kuwapa malezi bora watoto mama Happy John alisema ambaye ni mama wa nyumbani ”alisema Watoto wangu nilihahakikisha wapo katika mazingira mazuri na kuwapa muda wa kucheza.nashukuru kuwa hawajabadilika mpaka wamekuwa watu wazima wenye familia zao na kuziendeleza vizuri kama mimi nilivyowalea”. Wazazi wengi wamekuwa na imani potofu za malezi bora kwa watoto wao kwa kuwapa adhabu kali pale wanapokosea bila kujua kuwa mtoto ni mtu anayejifunza na anatakiwa kuelekezwa ili na yeye aweze kujua.

Kumpa mtoto adhabu kali si kumfundisha ila ni kumtia sugu kwa sababu itafikia wakati amezoea kupigwa hivyo haogopi kufanya
kosa lolote na anajijenga katika hali ya kutosikia.

Malezi bora kwa mtoto ni pamoja na kumpa elimu bora ambayo inamkuza kiakili na anaweza kujiandaa vema katika maisha yake ya baadaye ikizingatiwa kuwa elimu ni ufunguo wa maisha .

Mzazi akijua kuwa mtoto niTaifa la kesho,elimu ndio nguzo kuu katika hilo kwa sababu katika elimu tunapata mawaziri,raisi wafanyabiashara pamoja na wakulima walioelimika ambao watasaidia kuinua Taifa lao na maisha yao ya kifamilia.

Kutompa mtoto elimu kunasababisha kwanza kudumaa kiakili mtoto anakosa uwezo mkubwa na kuamua mambo hata kwa maisha yake anakuwa mtu wa kuamuliwa na inakuwa rahisi kwake kuvutwa katika vikundi vya ajabu.

Tukiangalia asilimia kubwa ya vijana waliojiunga katika vikundi vya wavutaji wa bangi,wizi,ujambazi na mambo mengi na kujikuta wanakaa bila kazi wala hawana wanalolifikiria katika kujijenga na hayo ni makosa ya wazazi,Mzazi anapofikiria kuwa mtoto anatakiwa ajue uwezo wake kuwa anaweza kuzaa watoto ambao ataweza kuwalea na kuwapa elimu bora nasi kuzaa tu watoto wengi ambao hataweza kuwalea na kuwapa elimu bora,hivyo mzazi anatakiwa azae watoto atakaoweza kuwalea na kuwapa elimu ya msingi.Katika makundi mabaya hayo ya wavutaji bangi,wezi majambazi na wenye kukosa mwelekeo wa maisha si wote ambao hawakuwapa malezi na elimu bora kutoka kwa wazazi.kila mzazi anapenda kumpa mtoto wake malezi na elimu bora ili na yeye aweze kujitegemea baadaye.

Watoto wengi wanaharibrika wanapokuwa shule hapo ndipo wanajiunga na makundi ya ajabu na kujikuta wakifanya mambo ambayo badala ya kujijenga wanaharibu maisha yao bila kufikiria familia zao zinajinyima ili wao wapate elimu.
Kama wazazi wanatakiwa kuwaeleza mapema watoto wao mambo ambayo ni mabaya yanayoweza kuatarisha maisha ya watoto wao wakiwa majumbani na mashuleni ili waweze kuyafahamu na kuyaepuka.

Kwa watoto wa kike wanaopata mimba katika umri mdogo wazazi wanatakiwa kuliepuka hilo kwa kuwaeleza watoto wao mapema na kuwafanya wasione tofauti ya urafiki kwa wanaume na wanawake.

Wazazi wengi wanawajengea watoto wao utofauti kati ya mwanamke na mwanaume kwa kuwakataza watoto hata kuongea na wanaume bila kujua wanawajengea fikra tofauti watoto na kuwasababisha kutaka kujua utofauti huo na ndipo wanapotenda vitendo visivyo kubalika katika jamii.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s